Klabu ya soka ya Southampton imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya
kombe la ligi zamani likijulikana kama Capital One baada ya kuifunga
Liverpool kwa jumla ya mabao 2-0 katika michezo miwili waliyoicheza.
Katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe hilo uliofanyika usiku
wa Jumatano hii, Liverpool walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa
Anfield na walifungwa 1-0 na Southampton kwenye dakika ya 90 huku goli
hilo likifungwa na Shane Long.
Wakati huo huo katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa
Januari 11 mwaka huu katika uwanja wa St. Mary’s unaomilikiwa na
Southampton walifanikiwa kuifunga Liverpool kwa bao 1-0 kupitia kwa
mchezaji wake Nathan Redmond.
Sasa timu hiyo inamsubiri mshindi katika fainali itakayochezwa kwenye
uwanja wa Wembley Februari 26 kati ya Manchester United na Hull City
ambao wanacheza nusu fainali yao ya pili Alhamisi hii huku mechi kwa
kwanza Man United ilifanikiwa kushinda maba 2-0.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment