Moja kati ya vitu au maamuzi yaliyoingia kwenye headlines ni kuhusiana na refa wa mchezo wa fainali ya Club bingwa dunia kati ya Real Madrid dhidi ya Kashima, mchezo ambao ulimalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa goli 4-2 na kutwaa taji hilo la Ubingwa.
Refa mzambia Janny Sikazwe alishindwa kumuonesha kadi nyekundu Sergio Ramosbaada ya kuwa tayari alimuonya kwa kadi ya njano dakika ya 55 ya mchezo kwa kosa la kwanza na beki huyo kurudia tena kosa, Sikazwe aliingia kwenye headlines baada ya kujisach kwa sekunde kadhaa akitaka kutoa kadi lakini baadae akaahirisha kitendo ambacho kimefanya wengi waamini kuwa alipendelea.
Kwa mara ya kwanza Janny Sikazwe ameweka wazi sababu iliyomfanya abadili maamuzi ya kumuonesha kadi ya pili ya njano Sergio Ramos“Tulishindwa kuelewana au naweza kusema tuli miss-communication kati yangu na msaidizi wangu aliniambia kupitia earpice kuwa faulo ile haikustahili kadi”>> Janny Sikazwe
0 comments:
Post a Comment