SIMULIZI | DOKTA SIUMWI HUKO | SEHEMU YA TANO

MSIMLIAJI: Kuluti MC
 OGELEA NAYO SASA; 
Kila mara Dokta Kisarawe hakuacha kumkumbuka Sulee;!

"Dah, yule ni mwanamke bwana," aliwaza Dokta Kisarawe jioni moja akiwa amejipumzisha.

"Halafu, si nilimwambia aje baada ya siku tatu;?," aliendelea kujiuliza maswali mengi.

"Eeh bwana; Ina maana kesho yupo hapa; Afadhali, kesho nitabimbilika naye tena" akaendelea kujikumbusha mwenyewe ndani ya chumba hicho.

"Twende mbele, turudi nyuma, aisee yule ni demu; Na hata muumba aliposema nitakufanyia msaidizi, alimaanisha yule; Kweli tena, fuatilia sana," Dokta Kisarawe akazidi kuzama kwenye mawazo hayo ya kujibizana na nafsi yake.

Dozi kali ya mchuzi wa pweza na karanga mbichi kwa wingi alizokuwa akizitumia Dokta Kisarawe, ziliendelea kumuweka sawa kwa ajili ya mechi kali ya kukata na shoka siku atakapokutana na Sulee.

"Mume wangu si unakumbuka dokta alisema nirudi baada ya siku mbili?" Sulee alimuuliza mumewe baada ya siku hiyo kufika.

"Kha! sasa mimi na wewe nani anapaswa akumbuke?," Masofa alimjibu kwa mkato na sauti ya kishari.

"Wote" Sulee naye akajibu kishari huku akimtupia jicho."Halafu wewe siku hizi mtata sana;"

"Nakumbuka basi, unasemaje?"

"Basi ni leo"

"Sasa ulikuwa unauliza au kunitaarifu?" Masofa alijibu lakini safari hii akiwa; siriasi’ zaidi.

Maisha ya Sulee na Masofa ndani ya ndoa yao, yalikuwa yameshaanza kuingia dosari.

Hii ni kutokana na hali ya Sulee kutopata ujauzito.

Sulee alinyamaza na kuendelea na shughuli zake. Masofa naye akaondoka kwenda kwenye mihangaiko yake ya kila siku.

Jioni ilipofika, Sulee alijiandaa kwa ajili ya kwenda kuonana na Dokta Kisarawe, moyoni akiwa amepania sana kupata tiba ya uhakika.

Akaianza safari ya kuelelekea kwenye zahanati ya daktari huyo. Alipofika alimkuta akiwa na mwanamke mwingine ndani, ikabidi asubiri nje.

Dakika moja baadaye, yule mwanamke aliondoka na kumpa nafasi Sulee kumuona Dokta Kisarawe;

"Niambie jamani," alisema Sulee huku akipanua mikono yake ili kumruhusu Dokta Kisarawe amkumbatie. 
ITAENDELEA.............!!! TUNAPATIKANA KWA SIMU NO; +25571490303/ Whatsapp HII NAMBA NI KWAAJILI YA USHAULI AU MAONI YUU YA SIMULIZI ZETU
Share on Google Plus

About omary omary

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment