MSIMLIAJI: Kuluti MC
ILIPOISHIA
*Dokta Kisarewa akawa anasikilizia utamu wa mashairi ya Sulee kwa kufuatisha alivyokuwa akiimba.
*Muda wa sebene ukawadia, kila mmoja akamuweka sawa mwenzake, mechi kali ikaanza.
SASA ENDELEA.....
ILIKUWA ni furaha ya aina yake kwa Dokta Kisarawe japo kwa Sulee ilitegemea na biti kwani wakati mwingine aliisikia sauti ikimwambia;
"Lakini wewe ni mke wa mtu, unalijua hilo?"
Sulee alishindana na akili zake kuhusu hilo, lakini sasa mapigo ya Dokta Kisarawe yalimfanya asitishe kwa muda kuwaza mambo hayo na kumpa ushirikiano mzuri;
"Dokta," aliita Sulee lakini hakuitikiwa kwani dokta alijitahidi ili amalize haraka na kuwahudumia wagonjwa wengine.
Hivyo alijitahidi kupiga mipira ya karibu. Sulee alikuwa hoi, kwa sababu alisimama, miguu iligoma kufanya kazi, akataka kukaa kwenye kiti lakini nafasi hiyo haikupatikana kwa Dokta Kisarawe.
Ni Sulee huyohuyo ndiye aliyeanza kutangaza hali ya hatari golini kwake, dokta akambana vizuri zaidi ili kumkinga na anguko lolote;
"Dokta; dokta nipe mtoto basi," alisema Sulee akitaka kujitoa kwa dokta baada ya kupasua dafu lake lakini dokta ambaye alihamasishwa na lugha hiyo alimzuia na yeye akatangaza kushuka chini ya mnazi na kuvunja dafu lake, wote wakavunja madafu yao.
Mlio wa pangaboi ndani ya chumba hicho cha dokta ndiyo uliosikika pekee huku kila mmoja akiwa hana la kumwambia mwenzake. Sulee alikaa kwenye kiti na kuinamia meza, dokta alisimama, mkono mmoja ulishika sehemu ya juu ya suruali yake akiiziba njia.
"Wewe Sulee wewe, hivi kweli umekuja kutibiwa au kutibua?" Sulee alisikia sauti ikimwambia hivyo
"Nimekuja kutibiwa," eti Sulee aliijibu ile sauti kwa kujiamini.
Sasa alikaa vizuri, dokta naye alikuwa kwenye eneo lake la kiti akimwangalia mwanamke huyo, aliyeumbika sawa na mapenzi ya muumba.
Wote walijikuta wakicheka, lakini Sulee akakatisha kicheko kwa swali
"Hivi mfano dokta"
"Eee"
"Ikitokea nimepata mimba mtoto wa nani?"
"Si wa kwako!"
"Hutamtaka?"
"Ha! Nimtakie nini wakati mimi nina mke wangu na watoto watatu, nimtake mtoto wako sijitaki kwangu?"
"Kwa hiyo unaniahidi?"
"Nakuahidi Sulee wala usiwe na wasiwasi."
Siku hiyo Dokta Kisarawe hakumpa dawa yoyote Sulee, akamwambia akaishi kwa siku thelathini kamili halafu arudi tena
"Noo dokta, mume wagu ataniuliza dawa ziko wapi?"
"Oke oke, basi chukua hizi, akikuuliza muoneshe..." Dokta Kisarawe alimpa Sulee vidonge vya kutibu mifupa, maarufu kwa jina la indosidi'.
"Hapo sawa."
Sulee aliondoka akiwa mwepesi sana, alitembea kwa madaha kurudi nyumbani kwake.
*************
Usiku wakiwa kitandani, mume wake alimuuliza;
"Vipi hospitali?"
"Nilikwenda."
"Walikupa dawa?"
"Ndiyo."
"Dawa gani?"
"Mi sizijui, sijui zinaitwaje!"
"Ziko wapi?"
"Sulee alitoka kitandani kwenda kuzichukua, akampa mumewe
"Hizi siyo za kuongeza damu?"
"Mi sijui, alisema niwe nameza vidonge viwili kwa siku mpaka mwezi mmoja uishe halafu niende tena."
"Sawa. Tutaona, kama hakuna matumaini itabidi tuachane naye," alisema mwanaume huyo akiwa amelala anaangalia juu.
************
Mwezi mmoja na siku mbili, siku hiyo Sulee alijiandaa vilivyo, si kama anakwenda kwa daktari kupata tiba ila anakwenda kwa mpenzi wake. Kama mumewe angekuwepo nyumbani angemzuia kuvaa alivyovaa
"Hapa niko sawa, mwenyewe akiniona atajua mimi ni mwanamke wa nguvu. Lakini Dokta Kisarawe naye, mh! Sijui alikwenda chuoni!"
Sulee alikuta wagonjwa wengine, akapanga foleni akiwa ni mtu wa kumi na saba mpaka kuingia chumba cha daktari. Alipita nesi
"Samahani anti, mwambie Dokta Kisarawe nipo hapa nje."
"Mh! Unadhani ataweza kuwaacha wenzako wote hawa akakuwahi wewe tu?" alihoji yule nesi.
"Sijasema awaache, nimekwambia mwambie nipo hapa nje."
"Umesema nani vile?"
"Sulee."
"Haya, subiri."
Nesi aliingia kwa dokta, aliweka cha kuweka kabla hajatoka akamwambia
"Kuna dada anaitwa Sulee, anasema amefika."
"Kwa hiyo?"
"Kasema nikwambie."
"Oke, mwambie umeshaniambia, asubiri. Yeye anadhani ni wa maana kuliko wenzake siyo?"
Nesi alitoka akafunga mlango huku macho yake yakikutana na macho ya Sulee
"Nimemwambia anti, lakini hajanijibu kitu."
Sulee kuna kitu kiligonga kichwani mwake;
"Au wanawake wote hawa ni wake, kwa hiyo kila mmoja ana umuhimu kwake? Maana kama mimi tu ndiyo mtu wake angetoa jibu lolote lile, isitoshe hatujaonana siku nyingi, mwezi na kitu sasa."
"Aingie mwingine," alisema Dokta Kisarawe akiwa amesimama mlangoni, alikutana macho na Sulee lakini hakuonesha uchangamfu wowote ule.
Dakika tano baada ya huyo mwanamke kuingia, vicheko na kugongeana mikono kulisikika kutoka kule ndani.
ITAENDELEA…TUNAPATIKANA KWA SIMU NO; +25571490303/ Whatsapp HII NAMBA NI KWAAJILI YA USHAULI AU MAONI YUU YA SIMULIZI ZETU
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment