MSIMLIAJI: Kuluti MC
GALAGALA NAYO SASA....
"Sasa mbona umekaa kimya, umenielewa;?" aliuliza tena Masofa akiwa amemkazia macho Sulee aliyekuwa bado amemtumbulia macho ya mshangao.
"Mmmh!," aliguna Sulee kabla ya kukubaliana na uamuzi wa mumewe, hapo moyoni alibaki na maswali mengi juu ya hali itakavyokuwa baada ya kufika kwa dokta siku inayofuata.
"Sawa," aliitikia huku akitingisha miguu mahali alipokuwa amekaa.
"Sawa, ndiyo nini;?"
"Kha!, si nimekubaliana na ulichosema," alisema Sulee huku akimwangalia mumewa kwa jicho la usinichoshe bwana'.
Masofa alibaki kimya kidogo, akaanza kuondoka kuingia chumbani huku akigeuka na kumwangalia Sulee.
Muda mfupi badaye, Sulee aliungana na mumewe chumbani ambapo bila hata kuvua nguo alijitupa kitandani.
"Aah, nianche bwana" alikuwa ni Sulee akimjibu mumewe aliyekuwa bize kwa kumshika sehemu mbalimbali za mwili hasa maeneo ya nyuma akiomba kutafuna tunda.
"Sasa nikuacheje jamani mke wangu?"
"Mimi nimechoka bwana;"
"Umechoka na nini"
"Kha! si kazi jamani, au watu huchoka na nini?"
Masofa hakujibu kitu zaidi ya kusitisha alichokuwa anakiomba.
Walipitiwa na usingizi hadi asubuhi ambapo Masofa alikuwa wa kwanza kuamka kabla ya Sulee aliyekuwa bado akiufaidi usingizi wa asubuhi uliokuwa ukisindikizwa na kibaridi cha alfajiri.
Masofa alijiandaa na kuelekea kazini, hakutaka kumsumbua Sulee akihofia mzozo usiokuwa na maana kwani aliyakumbuka vyema majibu yake ya jana.
******
Sulee aliendelea kulala hadi saa tatu na nusu aliposhituka ghafla. Akakurupuka na kukimbilia bafuni ambako alioga kabla ya kuanza kuandaa kinywaji.
Akiwa anakunywa chai, ghafla mazungumzo na majibizano yake ya jana na mumewe Masofa yakaanza kujirudia kichwani mwake.
"Haya, niambie huyo dokta amesema nini;?"
"Kwa leo amenipa ushauri tu wa kisaikolojia, amesema nirudi kesho muda kama wa leo," .
"Mm!, ina maana leo amekupa usahauri tu;?"
"Ee mume wangu;"
"Inabidi kesho twende;"
Kufika hapo, Sulee akaishiwa nguvu kimtindo.
"Sasa huyu naye anataka twende wote kwa dokta ili iweje?, wengine wanasumbuliwa na wivu, sasa kama yeye kazi hawezi si awaachie wenzake", aliwaza Sulee.
Akaendelea na majukumu mengine kama mama wa nyumbani, huku moyoni akiombea mumewe apatwe na dharura yoyote ili asiende naye kwa Dokta Kisarawe!
Mawazo yakampeleka hadi kwa Dokta Kisarawe ambaye tayari hisia za mapenzi zilishaanza kuchipuka baada ya kupatiwa raha ya ajabu jana yake.
"Nakupenda, nakutaka, nakuhitajiiii;.moyo wangu wakuwazaaa; mpenzi uko mbali namii" Sulee alijikjuta akiimba wimbo huo wa Lady Jay Dee uitywao Distance baada ya hisia juu ya Dokta Kisarawe kuzidi kumuwaka vibaya"
Hatimaye muda wa mumewe kutoka kazini uliwadia, ambapo maandaliazi ya kwenda kwa dokta yakaanza.
Ilipotimu saa moja na nusu, Masofa akiwa na mkewe walikuwa njiani kuelekea kwa Dokta Kisarawe.
Wakamkuta dokta akiwa peke yake kwenye chumba chake akiwa bize na ukaguzi wa mafaili mbalimbali ya wagonjwa.
Dokta Kisarawe alipomuona Sulee, mapigo ya moyo wake yakaongezeka, ikabaki kidogo tu aropoke jambo ambalo lingeharibu kila kitu.
"Jamani hon," alijikuta akikomea njiani japokuwa lile neon hon alitaka kutamka honey, lakini akajikuta akibadili haraka baada ya machale kumcheza haraka.
"Hata haujachelewa, aisee unazingatia sana muda;"
"Kawaida tu dokta" alijibu Sulee huku akijifanya kuvaa sura ya ubize kidogo.
"Ehee, naona umekuja na mgeni;"
"Siyo mgeni, huyu ndiye mume wangu"
"Ooh, karibu sana"
"Ahsante"aliitikia Masofa huku akimuangalia Dokta Kisarawe kwa jicho la "si utoe tiba tuondoke."
"Dokta Kisarawe naye akamwangali kama anayesema "Mbona umekaa kitemi sana."
"Ok, sasa sikiliza anti, nadhani jana uliyaelewa maelekezo yangu"
"Ndiyo dokta"
"Kuna dawa nitakupa kwa leo, ambazo utazitumia kwa siku tatu mfululizo kabla ya kurudi tena"
"Sawa, dokta".
Dokta Kisarawe akainama na kutoa kopo f'lani lililokuwa na dawa za vidonge, pamoja na zingine za maji!
"Hizi dawa ni muhimu sana, katumie kwa mtindo niliokuelekeza jana"
"Sawa."
Baada ya maelekezo hayo, waliagana kwa kupeana mikono huku Dokta Kisarawe akimpa moyo Masofa kuwa mkewe atapona na kuondokana kabisa na tatizo la kutozaa.
"Usijali, mkeo atapona tu"
"Ahsante sana dokta" alisema Masofa huku akipeana mkono.
Wakaachiana mikono lakini Dokta Kisarawe akawa anamtupia jicho Sulee aliyekuwa kimya muda wote.
***********
Toka siku hiyo, Dokta Kisarawe akawa anashinda akila karanga pamoja na kunywa mchuzi wa pweza kwa wingi, yote hiyo akiwa amempania Sulee atakapokuja siku ya tatu, kwani aliamini kwa vyovyote vile ni lazima aende peke yake.
ITAENDELEA.............!!! TUNAPATIKANA KWA SIMU NO; +25571490303/ Whatsapp HII NAMBA NI KWAAJILI YA USHAULI AU MAONI YUU YA SIMULIZI ZETU

0 comments:
Post a Comment