Adebayor kujiunga yanga ?

Kiungo wa zamani wa Real Madrid, Arsenal na Monaco Emmanuel Adebayor anatajwa kuwa muda wowote kuanzia sasa atajiunga na klabu ya Yanga ya  Dar es salaam kwa mkataba mnono.

Taarifa zilizotufikia zinamtaja nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Togo kuwa atajiunga na timu hiyo hili waweze kutetea ubingwa na kujiandaa na michuano ya kimataifa ya klabu bingwa Afrika.


Adebayor anataka kujiunga na wana-Jangwani hao ikiwa ni siku chache baada ya timu yao ya Taifa ya Togo kutolewa katika michuano ya AFCON.

Adebayor kama atajiunga klabu hiyo ya Yanga atakuwa mchezaji wa kwanza kutoka ligi ya mabingwa ulaya kuja kucheza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Share on Google Plus

About omary omary

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment