TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA 25/12/2016

WENGER KUSUBIRI HADI MSIMU UISHE AONGEZE MKATABA

Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger yupo tayari kusubiri hadi msimu uishe ili kusaini  mkataba mpya na Washika bunduki' hao wa London.

Wenger ambae mkataba wake unaisha mwaka 2017 alijiunga na Arsenal miaka 20 iliopita amesema yupo tayari kusibiria mkataba mpya mpaka msimu wa 2016/17 umalizike.

"Daima nishasema nitafanya maamuzi wakati huo klabu ipo huru pia sio kwasababu nimekaa hapa kwa mda mrefu" Wenger aliyaambia magazeti ya Uingereza.

Wenger ameiongoza Arsenal kutwaa mataji tisa tangu atue klabuni hapo ila taji la ligi kuu nchini Uingereza wakiwa wameshinda mara ya mwisho mwaka 2004.

JUVENTUS WAMTAKA KROOS


Klabu ya Juventus ya Italia imeanza mchakato wa kuweza kupata saini ya kiungo Mjerumani na Real Madrid Toni Kroos.

Juventus ambayo imemsajili Miralem Pjanic kutoka As Roma ili kuongeza nguvu katika kiungo hajatosheleza mahtaji ya timu kwani wanahitaji mtu ambaye ana uwezo kama alivyokuwa Andrea Pirlo.

Kroos ambaye amesaini mkataba mpya utakaomuweka hadi mwaka 2022 wenye thamani isiopungua paundi milioni 300 ambayo itawawia vigumu Juventus kumpata kiungo huyo kutokana na thamani ya mkataba wake japokuwa  hawajakata tamaa.

VAN DIJK HAUZWI WASEMA SOUTHAMPTON

eneja wa klabu ya Southampton Claude Puel amekiri kuwa beki  Virgil Van Dijk bado yupo kwenye mipango yao ya baadae licha ya kuhusishwa kutakiwa na timu mbali mbali  barani Ulaya.

Puel akiongea na vyombo vya habari alisema "Kwa Virgil ada ya uhamisho wake itakua vile vile katika miaka miwili au mitatu na atakaa nasi kwa miaka hiyo.Ni mchezaji muhimu kwetu na ni nahondha mzuri kwasababu anauelewa uongozi".   

Manchester City imemfanya Van Dijk mwenye miaka 25 kuwa chaguo la kwanza katika usajili wa mwezi Januari huku Klabu za Chelsea, PSG na Liverpool zikihitaji huduma ya beki huyo raia wa Uholanzi. 

Southampton itaendelea kumtegemea beki huyo wikii hii itakapomenyana na Tottenham Hotspur wakijaribu kutafuta nafasi za juu ili waweze kushiriki michuano mikubwa barani Ulaya.



Share on Google Plus

About omary omary

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment