Kikosi cha Simba kimeendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.
Simba inaongoza kwa tofauti ya pointi nne sasa dhidi ya wapinzani wao wakubwa Yanga, ikiwa ni baada ya kufikisha pointi 41 wakati Wanajangwani wana 37.
Lakini kinachoonekana, kwamba Simba imeingia kwenye ‘ugonjwa’ wa kupoteza nafasi baada ya kupoteza nafasi zaidi ya tano za wazi katika mechi dhidi ya JKT.
Mabingwa watetezi Yanga walitenegeneza nafasi nyingi zaidi kuliko timu nyingine yoyote ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita. Lakini walizitumia kufunga chini ya nusu ya nafasi hizo.
Simba ilionyesha soka safi katika mechi ya jana licha ya umahiri wa JKT. Simba walitengeneza rundo la nafasi la umaliziaji ukawa tatizo kubwa.
Shiza Kichuya alipoteza zaidi ya nafasi mbili, Mo Ibrahim nafasi mbili, Muzamiru Yassin pamoja na kufunga alipoteza mbili, Pastory Athanas ambaye alionyesha kiwango kizuri naye akapoteza mbili.
Mwendo huo kawaida huongezeka kwa kasi kama haufanyiwi na kazi na unaweza kuwa na athari kwa kuwa timu hutakiwa kutumia zaidi ya asilimia 55 ya nafasi nzuri za kufunga ilizotengeneza.
0 comments:
Post a Comment