Siku kadhaa zimepita tangu superstar wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amzindue hotel yake ya pili kwenye mji mkuu wa Ureno, Lisbon, akisema ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu kumiliki hotel yake mwenyewe.
Mreno huyo alisafiri moja kwa moja hadi Lisbon baada ya Madrid kulazimishwa sare ya kufungana 1-1 nyumbani na Eibar kabla ya mechi za kimataifa ambapo baadae usiku alizindua Pestana CR7 Lisboa hotel.
“Nilipokuwa mdogo nilikuwa na ndoto ya kumiliki hotel yangu,” Ronaldo aliwaambia watu waliohudhuria uzinduzi wa Pestana CR7 Lisboa.
Hotel hiyo yenye vyumba 82 ni ya pili, ambapo tayari alifungua ya kwanza kwa ushirikiano na Pestana group kwenye mahali ambapo alizaliwa kwenye kisiwa cha Madeira huku akiwa na mipango ya kuzindua nyingine mbili mwaka 2017 kwenye jiji la Madrid na New York
Hotel Pestana CR7 Funchal Madeira
Hotel hiyo ambayo ipo eneo la Madeira imepambwa na vitu mbalimbali za Ronaldo ikiwa ni pamoja na jezi ambazo zinasaini yake.
Pestana CR7 Lisboa, Lisbon
Hotel hiyo mpya ambayo ipo Lisbon ambao ndio mji mkuu wa Ureno, ambako ndipo Ronaldo alianzia soka na timu yake ya utoto Sporting CP. Ipo mita 50 kutoka Prace de Comercio riverside square.
Cristiano Ronaldo aliizindua akiahidi itakuwa na utamaduni wa maisha yake halisi.
Gharama za kulala kwa usiku mmoja zinaanzia euro 200 ikiwa ndio kiasi cha chini huku kila chumba kikiwa na teknolojia ya kisasa.
0 comments:
Post a Comment