SIMULIZI | DOKTA SIUMWI HUKO | SEHEMU YA SABA

MSIMLIAJI: Kuluti MC
 ILIPOISHIA
"Aingie mwingine," alisema Dokta Kisarawe akiwa amesimama mlangoni, alikutana macho kwa macho na Sulee lakini hakuonesha uchangamfu wowote ule.

Dakika tano baada ya huyo mwanamke kuingia, vicheko na kugongeana mikono vilisikika kutoka kule ndani.

TIRIRIKA NAYO SASA...

Sulee akaamua kunyanyuka mahali alipokuwa amekaa na kusogea karibu kabisa na mlango.

Akawa anategesha sikio kusikia zaidi kinachoendelea ndani ya chumba cha Dokta Kisarawe.

Vicheko viliendelea kusikika, kugongeana mikono kukazidi kuchukua nafasi kubwa....!

Sulee alirudi hadi alipokuwa ameketi awali, nakuanza kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.

"Hivi, wanaweza kuwa wanafahamiana kweli...?"
"Kha, lakini nami bwana, sasa kama hawafahamiana wanawezaje kucheka na kugongesheana mikono namna hiyo...?"
"Kwa vyovyote vile watakuwa wanafahamiana tu, ngoja nifuatilie sana...!

"Sasa kama wanafahamiana, kuna uwezekano huyu dokta kuwa anatuchanganya...?"
"Yawezekana..."

"Lakini ni sisi wanawake yawezekana ndiyo tunajichanganya...," Sulee aliendelea kujisemea juu ya hali aliyoiona kwa siku hiyo.

"Ina maana kila mwanamke mwenye ugonjwa kama wangu, ni lazima atembee na huyu dokta ndiyo apone...?"
"Sasa kama ni hivyo atakuwa ametembea na wangapi?"

"Kama ndiyo mtindo wake, kwa nini sisi wanawake tusishituke?”

"Kuna uwezekano wanawake wengi wanajua, lakini nani wa kuvujisha siri kama anapokea dozi ya maana ya Dokta Kisarawe...? Halafu sasa unakuta wengi wao ni wake za watu, lakini sisi wanawake bwana...!

"Sisi wanawake siyo, wewe tufuatilie sana, siyo kwa sababu haiwezekani wote hawa tutembee na mtu mmoja na siri isijulikane...," maswali yakazidi kumchanganya Sulee mahali alipokuwa amekaa.

Lakini kwa wakati wote huo akiwa amekaa kwenye ile foleni, macho yake hayakuwa yanabanduka kwenye mlango wa ofisi ya Dokta Kisarawe...

"Lakini mimi naye bwana, sasa nimethibitishaje kuwa ni wapenzi labda huenda wanafahamiana tu na umepita muda mrefu bila kuonana?"

"Lakini, kufahamiana gani huko wanacheka hadi kugonganisha mikono kwa sana...?"

"Sasa kwani kugongeana mikono kuna maanisha nini...?," Sulee akazidi kujihoji na kujijibu mwenyewe, hali ilishaanza kuwa tete ndani yake. Moyo haukuwa na amani tena na kidonda cha wivu kilishaanza kumnyemelea.

"Yaani kweli mambo anayonifanyia Dokta Kisarawe, anaweza kumfanyia mwanamke mwingine kweli?"

"Eee, inawezekana kwani kama aliweza kwako ni kivipi asiwafanyie wengine...," ilisikika sauti ikimjibu kutoka upande wa pili wa moyo wake.

"Ila kweli, hilo nalo neno."

Sulee aliendelea kujihoji na kujijibu mwenyewe. Hali haikuwa hali. Dokta Kisarawe alikuwa amemuingia moyoni mwake, sasa alikuwa haambiliki wala kusikia chochote juu yake.

"Haya mapenzi bwanaaa, hayana maana....," wimbo wa Diamond ulisikika masikioni mwake baada ya kushindwa kuhimili vishindo vya maumivu ya wivu wa mapenzi.

Muda mfupi baadaye, Sulee aliamua kusogea tena karibu kabisa na mlango wa ofisi ya Dokta Kisarawe. Lengo la safari hii ni kusikia nini kilikuwa kikiendelea ofisini humo.

Sulee alishituka baada ya kusikia sauti za kunong'ona kwa chini sana tofauti na awali ambapo Dokta Kisarawe na mteja wake walikuwa wakizungumza kwa sauti ya juu.

Safari hii alisikia watu wakibusiana, moyo ukazidi kumuuma...

Akajishika kifuani kwa upande wa kushoto ulipo moyo, mapigo yakazidi kumuenda mbio.

Dakika mbili baadaye, alianza kusikia miguno na sauti ya meza na kiti vikisogea...Moyo ukazidi kumuuma kuliko kawaida.

"Kuchiii.....kwaguuu...vegeeee....vegeeee.....vigi...vigiiiii....," milio ya kiti na meza viliendelea kusikika na kuzidi kumpa maswali mengi sana Sulee...

Mbali na milio ya samani hizo, miguno na mihemko ya chini ikazidi kusikika, kila dalili ya watu kula mua ikawa inajionesha wazi...

Sulee akashindwa kuvumilia, akarudi kwenye kiti. Dakika tano baadaye yule mwanamke akatoka. Dokta Kisarawe naye akatoka nje na kumuita mwanamke mwingine. Lakini wakati akimuita mtu mwingine, macho yake na ya Sulee yalikutana lakini hakuonesha dalili yoyote ya kumchangamkia (Sulee). Hali hiyo ikazidi kumchanganya kabisa Sulee.

Kuna kipindi akataka kuondoka lakini akazidi kujipa moyo na kuendelea kusubiri aone hatma ya mchezo wa siku hiyo.

"Kha, au kuna kitu nimemkosea ndiyo maana kachukia namna hii, au niondoke? Lakini nikiondoka wakati nimeshafika hapa itakuwa si busara. Ngoja niangalie mwisho wa hii sinema...," akawaza moyoni Sulee.

Hatimaye wote wakaisha na kubaki kwenye benchi peke yake. Akadhani sasa zamu yake imewadia. Lakini alishangaa kumuona Dokta Kisarawe akitoka huku akifunga mlango wa ofisi yake kwa ufunguo.

Kuona hivyo, Sulee akahamaki na kumuuliza kulikoni iwe hivyo na vipi kuhusu tiba yake kwa siku hiyo?

"Haa, sasa Dokta mbona unaondoka vipi kuhusu mimi jamani...?

"Kuhusu wewe nini tena..."
"Si tiba yangu..."
"Ipi..."
"Ya siku zote, ina maana umesahau kabisa...?"
"Hebu acha maneno yako wewe...," alijibu Dokta Kisarawe huku akimalizia kufunga kufuli la mlango.

ITAENDELEA.....
TUNAPATIKANA KWA SIMU NO; +25571490303/ +255752292473 Whatsapp HII NAMBA NI KWAAJILI YA USHAULI AU MAONI YUU YA SIMULIZI ZETU
Share on Google Plus

About omary omary

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment