Simba ambayo inaanza michuano ya Kombe la Mapinduzi leo, imesema itaichukuliwa michuano hiyo kwa uzito kama sehemu ya morali.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya usajili, Kassim Dewji amesema wanaamini hakutakuwa na utani.
“Unajua kufanya vizuri kunaongeza hali ya kujiamini, kunaongeza morali. Sisi tunataka kushinda na kufanya vizuri kabla ya kurejea kwenye ligi.
“Wachezaji wanajua na benchi la ufundi linajua. Tutafurahi kama wakipambana na kurejea na ushindi mkubwa ambao utakuwa morali kwenye ligi kuu,” alisema.
Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara. Maana yake watakaa nje ya ligi hiyo kwa wiki mbili hasa kama watasonga zaidi katika Mapunduzi Cup inayofanyika visiwani Zanzibar.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment