NAHODHA wa Azam, John Bocco, amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Simba Jumamosi ijao hautakuwa mwepesi huku akiamini vinara hao wa ligi watataka kulipiza kisasi.
"Haimaanishi kwa sababu tuliwafunga kwenye mchezo wa fainali wa kombe la mapinduzi basi mambo yatakuwa mepesi kwetu hapana, naamini kabisa Simba wamejipanga kama ambavyo na sisi tumejipanga..., mchezo utakuwa mgumu," alisema Bocco.
Alisema, kwa sasa wao kama wachezaji watahakikisha hawapotezi mchezo ili kuweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu.
Mchezo huo wa Jumamosi utakumbushia fainali ya Kombe la Mapinduzi iliyochezwa Januari 13 mjini Zanzibar na Azam kutwaa ubingwa huo kwa mara ya tatu baada ya kushinda kwa goli 1-0.
Goli hilo pekee lilifungwa na kiungo mkabaji, Himid Mao na kuifanya Azam kufikia rekodi ya Simba ya kutwaa ubingwa huo mara tatu.
0 comments:
Post a Comment