Takwimu zinaweza kutengenezwa ili kuleta maana au kushawishi jambo fulani lakini sio kipindi ambacho mhusika ni mzee mwenye akili timamu anayefahamika kama Michael Carrick. Takwimu haziwezi kuongopa na hii inatokana na umuhimu wake anaouleta kwenye klabu ya Manchester United.
United wamefanikiwa kushinda asilimia zaidi ya 47 za michezo aliyocheza mchezaji Michael Carrick kuliko ambazo hajacheza kwenye eneo lao la kiungo. Katika msimu huu United wameshinda asilimia 83 ya michezo aliyohusika, 10 kati ya 12.
Michezo mingine miwili aliyocheza imetoka kwa sare, zikiwemo zile mechi ambazo vilabu vya Arsenal na Everton vilifanikiwa kusawazisha dakika za mwisho. Manchester United wamefunga mabao 30 akiwepo na kuruhusu 9 tu.
Uwezo wa Michael Carrick umeisaidia klabu ya Manchester United kiasi cha kuleta ubora na kuelewana kati ya wachezaji Phil Jones na Marcus Rojo.
Bila kusahau kuwa hata uwezo wa Paul Pogba umeanza kuzaa matunda kipindi ambacho Carrick amerejea kikosini na Jose Mourinho kuamua kukubali yaishe. Hii pia inaweza kuwa sababu ya kushawishi kuongezwa kwake mkataba.
MANCHESTER UNITED WAKIWA NA CARRICK
Michezo: 12
Kushinda: 10
Sare: 2
Kupoteza: 0
Magoli Yaliyofungwa: 30
Magoli yaliyoruhusiwa: 8
Asilimia ya ushindi: 83%
Asilimia ya kufungwa: 0%
MANCHESTER UNITED BILA CARRICK
Michezo: 14
Kushinda: 5
Sare: 4
Kupoteza: 5
Magoli Waliyofunga: 14
Magoli waliyoruhusu: 15
Wastani wa Ushindi: 36%
Wastani wa kupoteza: 36%
Ni wazi kuwa kocha wa Manchester United, Jose Murinh hathitaji kuna Carrick akiondoka na badala yake atahitaji kumwongeza mkataba.
Sio hivyo tu bali hata vijana wa Manchester United wenye umri wa chini ya miaka 14 nao wananufaika na uwepo wake huyu ambaye amepewa majukumu ya kuwasimamia.
Carrick anatumia muda wake mwingi kuweza kufundisha illi aweze kufanikiwa kupata leseni A ya ukocha ya UEFA.
Carrick amehusika katika kucheza na viungo wengi mpaka leo katika klabu ya Manchester United, mmoja wao akiwa ni Paul Scholes. Kuna orodha ndefu sana mpaka ufikie jina la Paul Pogba na hii inaweza kukupa sababu ya kwanini Manchester United na viungo wataendelea kunufaika.
Carrick anamlisha anavyotaka, anampa uhuru anaojisikia na sasa Pogba anacheza soka la maisha yake akiwa na Manchester United.’
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment