Hazard, Costa waweka rekodi mpya Chelsea ikiua 3-0 Darajani

Chelsea wamefufua matumaini ya mbio za kuwania ubingwa wa Premier League baada ya kuwafunga Mabingwa Watetezi Leicester City mabao 3-0, mchezo uliofanyika Stamford Bridge.
Magoli ya Chelsea yamefungwa na Diego Costa dakika ya 7 baada ya kupata pasi kutoka kwa Nemanja Matic.
Chelsea walipata bao la pili kupitia kwa Eden Hazard dakika ya 33 baada ya kazi nzuri kutoka kwa Pedro Rodriguez.
Bao la tatu la Chelsea limefungwa na Victor Moses dakika ya 80 kufuatia kazi nzuri ya Chilobah.
Takwimu muhimu
  • Leicester City imekuwa timu ya kwanza kama Mabingwa Watetezi kupoteza mechi zao zote nne za mwanzo za ugenini tangu ilivyotokea kwa Blackburn msimu wa 1995-96.
  • Costa amefunga magoli 39 na kutoa assists 11 kwenye mechi 62 za EPL.
  • Tangu acheze mchezo wake wa kwanza tangu asajiliwe na Chelsea, Eden Hazardndiyo mchezaji kiungo mwenye magoli mengi kuliko yeyote EPL (44).
Share on Google Plus

About omary omary

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment