Serikali imezicharukia Simba, Yanga, Azam FC na timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ambazo wachezaji wao hawajapata vibali vya kufanya kazi nchini.
Ofisa Uhamiaji wa jiji la Dar es Salaam, John Msumule amesema mchezaji yoyote ambaye atakuwa hajakamilisha suala la kibali cha kazi asithubutu kucheza wala kukaa kwenye benchi.
“Hili ni agizo, kama mchezaji hana kibali cha kazi asifanye kazi na wala hakutakuwa na utani. Wote wanajua taratibu ni zipi, basi zifuatwe,” alisema.
Leo mchana, Yanga na Simba walikuwa wakihaha katika ofisi za Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam kuhakikisha wanapata vibali hivyo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit na Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele walionekana kwenye ofisi hizo.
Lakini baadaye, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba naye alifuatia ikionekana kila upande ulikuwa ukihaha kukamilisha taratibu hizo.
0 comments:
Post a Comment