BAADA ya kuwa katika kiwango duni katika siku za hivi karibuni hatimaye usiku wa kuamkia leo Paris Saint-Germain imewapa mashabiki wake zawadi nzuri ya Christmas baada ya kuifumua Lorient mabao 5-0 katika mchezo wa mwisho wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa [Ligue 1] tayari kwa mapumziko mafupi ya kupisha majira ya baridi.
Katika mchezo huo uliochezwa Parc des Princes,mabao ya Paris Saint-Germain yamefungwa na Thomas Meunier, Thiago Silva, Edinson Cavani, Lucas Moura na bao la kujifunga la Zargo Toure.
Katika mchezo mwingine Nice ililazimika kumaliza mchezo wake dhidi ya Bordeaux ikiwa na wachezaji tisa uwanjani baada ya Mario Balotelli na Younes Belhanda kuonyeshwa kadi nyekundu za moja kwa moja katika matukio mawili.Mchezo huo uliisha kwa sare ya kutofungana.
Katika mchezo mwingine Radamel Falcao amefunga bao moja na kuiwezesha Monaco kuibuka na ushindi wa mabao 2-1dhidi ya Caen.Bao la pili la Monaco limefungwa na Tiemoue Bakayoko
0 comments:
Post a Comment