HAWANA BUSARA! : LWANDAMINA AWAPONDA WACHEZAJI YANGA

Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina ,  amesema hajafuraishwa na  tabia ya wachezaji wake kugomea mazoezi kwa sababu ya kucheweleshewa mshahara kwa siku chache.
Lwandamina amesema,  wachezaji wake walikosa busara na kushindwa kuupa nafasi uongozi kufanya majukumu yake kama inavyokuwa siku zilizopita na walichofanya wamekurupuka na kuitia aibu klabu.
“Walipaswa kujiuliza matukio kama hayo ya kucheleweshewa mshahara yamejitokeza mara ngapi katika msimu huu na mbona stahiki zao nyingine wanapata kwa wakati ikiwemo posho tena bila kujali matokeo ya uwanjani vipi wao wanashindwa kutimiza moja ya majukumu yao yaliyopo kwenye mkataba,” alisema Lwandamina.
Kocha huyo raia wa Zambia alisema kwa mtazamo wake wachezaji hawajaitendea haki Yanga, kwa sababu kama swala ni mshahara kuchelewa wangezungumza na meneja wa timu Hafidh Salehe pamoja na yeye na nahodha Haruna Niyonzima kwenda kuzungumza na uongozi na siyo kufanya hivyo walivyofanya.
Alisema kukosa mazoezi kwa siku mbili wakati timu ikiwa kwenye ligi hasa kubwa na wachezaji wanapaswa kulitambua hilo kwa sababu endapo watapoteza mchezo wao wa kesho dhidi ya African Lyon, wao ndiyo wanastaili kubeba lawama kwa sababu walijithamini wao na siyo kazi.
Mambo hayo yalimalizika na leo jioni timu hiyo imefanya mazoezi kujiandaa na mchezo wao wa ligi ambao utapigwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Kocha huyo ana kibarua kigumu cha kuitoa Yanga nafasi ya pili na kuipa ubingwa wa Tanzania Bara, ambao inaushikili kwa sasa baada ya kuutwaa mara mbili chini ya kocha Mdachi Hans Pluijm ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa timu hiyo.
Share on Google Plus

About omary omary

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment