Wachezaji wa Yanga, wamegoma kufanya mazoezi kwa siku ya pili mfululizo.
Wachezaji hao walianza kugoma kufanya mazoezi jana kwa madai ya kucheleweshewa mshahara wao kwa siku 19.
Lakini leo, wameshindwa tena kutokea mazoezini kwa mara nyingine huku mchezaji mmoja tu, Ally Mustapha ‘Barthez’ akionekana katika eneo la Uwanja wa Uhuru.
Basi la Yanga aina ya Yutong lilifika uwanjani hapo bila ya kuwa na wachezaji na baadaye likaondoka likiwa limewabeba makocha.
Tayari Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema wanalishughulikia suala hilo.
Lakini taarifa nyingine, zinaeleza, uongozi wa Yanga ulishawataarifu wachezaji kwamba wangelipwa leo fedha zao lakini ikaonekana wachezaji wamechukizwa na suala hilo kutotekelezwa.
Yanga inatarajia kucheza mechi yake ya pili ya mzunguko wa pili dhidi ya African Lyon, Ijumaa.
0 comments:
Post a Comment