Barcelona imeifanyia mauaji makubwa klabu ya daraja la pili ya Hercules baada ya usiku wa jana Jumatano kuichapa mabao 7-0 katika mchezo wa hatua ya mtoano [hatua ya 32 bora] wa kombe la Copa del Rey maarufu kama kombe la Mfalme.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Camp Nou,Barcelona ilijipatia mabao yake kupitia kwa Paco Alcacer, Lucas Digne,Ivan Rakitic, Rafinha na Arda Turan aliyefunga mabao matatu "hat trick".
Ushindi huo umeipeleka Barcelona katika hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 8-1.Ikumbukwe katika mchezo wa awali matokeo yalikuwa sare ya 1-1.
Katika mchezo mwingine wa Copa del Rey,mabao matatu matatu ya Luciano Vietto na Wissam Ben Yedder yameipa Sevilla ushindi wa mabao 9-1 dhidi ya Formentera
9-1.
Mabao mengine ya Sevilla yamefungwa na Pablo Sarabia aliyefunga mabao mawili na Ganso aliyefunga bao moja. Gabri aliipatia Formentera bao la kufutia machozi.Katika mchezo wa awali Sevilla ilipata ushindi wa mabao 5-1 hivyo imefuzu kwa jumla ya mabao 14-2.
0 comments:
Post a Comment