Shirikisho la soka barani Afrika CAF leo December 21 2016 lilichezesha droo ya timu zitakazoshiriki michuano ya kimataifa kwa mwaka 2017 ngazi ya vilabu, CAF wamechezesha droo hiyo na kupanga timu zote zitakazoanzia round ya kwanza na round ya pili.
Mabingwa watanzania timu ya Dar es Salaam Young Africans imepangwa kuanza kucheza na Ngaya de Mbe ya Comoro katika michuano ya Club Bingwa Afrika na ikifanikiwa kuitoa timu hiyo itacheza na mshindi wa mchezo kati ya Zanaco ya Zambia dhidi ya APR ya Rwanda.
Wakati Azam FC wao wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika, lakini watakuwa wanasubiri mshindi kati ya Opara United ya Botswana dhidi ya Mbabane Swallows.
0 comments:
Post a Comment