Bata ambalo lipo kwenye akili ya kila mpenda burudani kwasasa ni kuhusu Wasafi Beach Party ambayo inatarajiwa kufanyika pande za Jangwani Sea Breeze jumamosi ijayo ya tarehe 24 December.
Show ambayo inasimamiwa na team nzima ya WCB Wasafi. Kitu ambacho kinatrend katika show hiyo ni ujio wa warembo tofauti tofauti kutoka nchi za jirani ambao wanatarajiwa kuja kulinogesha bata hilo.
Mmoja kati ya warembo ambao wamekuwa wakisikika sana katika midomo ya watu kuhusiana na kudondoka katika show hiyo ni mrembo Huddah kutoka pande za 254 Kenya.
Sasa C.E.O wa WCB Wasafi mtu mzima Diamond Platnumz ameweka wazi kuhusiana na tetesi hizo na kudai kuwa Huddah ni mmoja kati ya warembo ambao watalinogesha bata hilo.
Mrembo mwingine ambaye ametajwa kunogesha siku hiyo ni mrembo Fabiola kutoka nchini Uganda ukweni kwa mtu mzima Diamond Platnumz.
Fabiola kwenye pozi la chumbani
0 comments:
Post a Comment