STAND vs African Lyon, chama la wana kuendeleza ubabe?

Stand-united-xi
Stand-united-xi
kucheza na stand katika uwanja wa kambarage ni sawasawa na kupigwa kabla ya pambano kwa sasa. stand imeimarika ipo vizuri kila idara licha ya kuumia kwa mshambuliaji wao chidiebere Abasalim wao haiwastui sana. stand pia wanashikilia rekodi ya kutokupoteza mchezo hata mmoja msimu huu kama walivyo simba sports club
african lyon wao wanaonekana wana bahati mbaya sana na timu za shinyanga kwani wamefungwa na mwadui mabao 2-0 katika mchezo uliopita na leo wanakutana na timu ambayo haijui nini maana ya kufungwa kwa msimu huu. kocha Bernado Tavares atakuwa na kibarua kigumu mno cha kujinasua katika aibu inayowanyemelea dhidi ya stand united
jambo pekee linalongojewa ni ile jeuri na kiburi cha mashabiki wa stand united waliyonayo msimu huu, msimu ambao wengi walitabiri kwamba stand itatetereka wengi walidhani kwamba stand itayumba baada ya migogoro na kuondokewa na mdhamini wake mkuu.
Share on Google Plus

About omary omary

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment