Mexime awaanzisha Mrwanda, Edo Christopher kikosi cha Kagera kuivaa Simba

Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Danny Mrwanda

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amewaanzisha kwa pamoja washambuliaji wa zamani wa Simba, Danny Mrwanda na Edward Christopher katika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya vinara Simba.
Chipukizi Mbaraka Yussuf ambaye alitolewa kwa mkopo na Simba msimu uliopita ameanzishwa kwenye safu ya ushambuliaji na kuwaacha wakongwe Themi Felix na Paul Ngwai wakisugua benchi.
Langoni atasimama Hussein Sharrif ambaye pia aliwahi kuchezea Simba bila mafanikio kabla ya kuamua kukimbia benchi na kurudi Mtibwa Sugar na baadae kutua Kagera Sugar.
Kikosi kamili: Hussein Sharrif, Godfrey Taita, Mwaita Salehe, Shaban Sunza, Suleman Mangongo, Ally Nassoro, Danny Mrwanda, Christopher Edward, Mbaraka Yusuf, John Chacha.
Akiba: Erick Kyaruzi, Paul Ngwai, Ally Ramadhan, Japhet Makwata, Themi Felix, Babu Ally
Share on Google Plus

About omary omary

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment