MAN CITY WAMTAKA ISCO
Kiungo wa Real Madrid Isco ametajwa kuwa mmoja ya wachezaji ambao kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kuwasajili kwenye kikosi chake.
Isco alijiunga na Madrid mwaka 2013 ameshindwa kujihakikishia nafasi katika klabu hiyo huku akianza katika michezo 10 pekee kwenye michuano yote walioshiriki.
City ambao wamekuwa wakimtaka nyota huyo tangu mwaka 2012 watatumia nafasi ya kukosa namba kwenye kikosi cha LOS BRANCOS ambapo kwa sasa amesitisha mazungumzo ya kusaini mkataba mpya klabuni hapo.
BARCELONA KUMNASA IVANOVIC
Klabu ya Barcelona imeendeleza jitihada zake za kutafuta beki wa kulia na sasa wamehamishia nguvu kwa wa Chelsea Branislav Ivanovic.
Barcelona imekua ikiwafuatilia mabeki mbali mbali kama Hector Bellerin ambaye alisaini mkataba mpya na Arsenal huku Srna nae akigoma kusaini kutokana maslahi madogo.
Ivanovic anategemewa kutimka Chelsea katika dirisha ili dogo la usajili kutokana na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kocha Antonio Conte.
CHICHARITO KUJIUNGA NA CHELSEA
Mshambuliaji wa timu ya Bayern Leverkusen ya Ujerumani Javier Hernandez 'Chicharito' anahusishwa na dili la kujiunga na Chelsea katika dirisha hili la usajili.
Chicharito alitimka Manchester United majira ya joto na kujiunga na Leverkusen amekuwa katika kiwango bora kilichowavutia Chelsea kuhitaji huduma yake.
Leverkusen wapo tayari kumuachia Chicharito kwa ada ya uhamisho isiopungua euro milioni 35.
VALLEJO KUREJEA MADRID
Beki wa Real Madrid aliye kwa mkopo katika klabu ya Eintracht Franfurt Jesus Vallejo anatarajiwa kurejea klabuni hapo baada ya mkopo kuisha huku Pepe akitaka kutimka baada ya mkataba wake kwisha.
Vallejo alitazamiwa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi wa mkopo ambapo uwezo wake alionyesha akiwa Liverkusen miamba ya Hispania wamekataa ofa ya kuongeza mwaka mwingine kwa mkopo na hivyo kutegemea kurejea juni 30.
Vallejo anategemewa kumrithi Pepe ambae amepata ofa kutoka klabu mbalimbali kutoka china huku mshahara wa euro milioni 10 kwa mwaka ukimvutia zaidi.
PSG WAMUANDALIA DAU COUTINHO
Liverpool ipo katika wakati mgumu wa kumzuia kiungo wake fundi Phillipe Coutinho baada ya matajiri wa Ufaransa timu ya Paris Saint Germain kuonesha nia ya kutaka kumsajili.
Coutinho yupo majeruhi tangu alipo umia katika mechi dhidi ya Sundeland katika ushindi wa mabao 2-0.
PSG wapo mbioni kupeleka dau la paundi milioni 44 ili kuishawishi Liverpool kumuachia kiungo huyo.
PSG wameungana na timu za Barcelona na Real Madrid katika kinyang'anyiro hicho cha kumpata nyota huyo.
0 comments:
Post a Comment