Benpol open about Collabo reasons for its delay by Chidinma
Kama una kumbukumbu vizuri naamini utakuwa unakumbuka kwamba mwezi may mwaka jana mkali wa RnB Tanzania Benpol alitusanua kuwa hautomalizika mwaka wa 2016 kabla ya kuachia ngoma akiwa kamshirikisha mwanadada Chidinma wa Nigeria.
Sasa tumeona kimya mpaka mwaka 2016 umemalizika na sasa tunaelekea mwishoni mwa mwezi january mwaka 2017 na collabo hiyo hatujaisikia!
Kipi kimejiri? Benpol amepiga story na Perfect255 na ametusanua kilichojiri na kusababisha collabo hiyo kushindwa kuachiwa kwa mwaka 2016.
“Kwanza Chidinma nimefanya nae ngoma mbili, kuna Moyo Mashine remix na pia kuna nyingine. Sasa Moyo Mashine remix tulichelewa timing, kwasababu plan zilikuwa remix iwe tayari kabla original haijatoka, lakini tukachelewa timing, alikuja kuituma ile part yake nafkiri ilikuwa ni November.”
Hayo ni machache tu kati ya mengi ambayo Benpol amefunguka kuhusiana na collabo hiyo na Chidinma. Play hii video hapa chini kumsikiliza mkali huyo akifunguka mwanzo hadi mwisho.
0 comments:
Post a Comment