U HEARD: Nyingine ya msanii aliyetapeliwa laki 5 ili wimbo wake upigwe redioni


December 20, 2016 kupitia U HEARD ya XXL ndani ya Clouds FM, Soudy Brown ameipata hii ya msanii aitwaye Super Ruby ambaye kwa mujibu wa Soudy amesema hajawahi kutoa wimbo wowote redioni isipokuwa alikuwa anatafuta mtu wa kumsaidia kusimamia nyimbo zake ili zichezwe redioni.
Soudy amezungumza na jamaa anayefahamika kwa jina la Becka ambaye alikutanishwa na msanii huyo na kumtaka ampe shilingi laki tatu ili amsaidie kuufikisha wimbo wake Clouds FM na kuutafutia ratiba ya kuchezwa redioni kila mara. 
“Hapana mimi sijamtapeli huyo kuna mtu wake na huyo msanii ndio walinifata mimi wakawa wanataka kusambaziwa nyimbo na mimi kuna dada niliunganishwa naye nikawapa hao kwahiyo wakawa wanawasiliana wenyewe, nakubali hela alinirushia ila kuna dada nilimpa” – Becka 
Msanii Ruby amesema kuwa ameshampa Becka pesa zaidi ya shilingi laki tano mpaka sasa ili nyimbo zake zianze kuchezwa Clouds FM lakini hakuna kilichofanyika na kila akijaribu kumpigia huyo jamaa hapokei simu zake japokuwa aliwahi kumrekodi kwenye maelezo yake ya mwanzo.
Kuipata FULL STORI Bonyeza play hapa chini usikilize
Share on Google Plus

About omary omary

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment