MICHAEL CARRICK: Dawa Inayoingia Damuni Kwa Manchester United


Takwimu zinaweza kutengenezwa ili kuleta maana au kushawishi jambo fulani lakini sio kipindi ambacho mhusika ni mzee mwenye akili timamu anayefahamika kama  Michael Carrick. Takwimu haziwezi kuongopa na hii inatokana na umuhimu wake anaouleta kwenye klabu ya Manchester United.
United wamefanikiwa kushinda asilimia zaidi ya 47 za michezo aliyocheza mchezaji Michael Carrick kuliko ambazo hajacheza kwenye eneo lao la kiungo. Katika msimu huu United wameshinda asilimia 83 ya michezo aliyohusika, 10 kati ya 12.
Michezo mingine miwili aliyocheza imetoka kwa sare, zikiwemo zile mechi ambazo vilabu vya Arsenal na Everton vilifanikiwa kusawazisha dakika za mwisho. Manchester United wamefunga mabao 30 akiwepo na kuruhusu 9 tu.

Bila kusahau kuwa hata uwezo wa Paul Pogba umeanza kuzaa matunda kipindi ambacho Carrick amerejea kikosini na Jose Mourinho kuamua kukubali yaishe. Hii pia inaweza kuwa sababu ya kushawishi kuongezwa kwake mkataba.

MANCHESTER UNITED WAKIWA NA CARRICK

Michezo: 12
Kushinda: 10
Sare: 2
Kupoteza: 0
Magoli Yaliyofungwa: 30
Magoli yaliyoruhusiwa: 8
Asilimia ya ushindi: 83%
Asilimia ya kufungwa: 0%
Michezo: 14
Kushinda: 5
Sare: 4
Kupoteza: 5
Magoli Waliyofunga: 14
Magoli waliyoruhusu: 15
Wastani wa Ushindi: 36%
Wastani wa kupoteza: 36%


Ni wazi kuwa kocha wa Manchester United, Jose Murinh hathitaji kuna Carrick akiondoka na badala yake atahitaji kumwongeza mkataba.
Sio hivyo tu bali hata vijana wa Manchester United wenye umri wa chini ya miaka 14 nao wananufaika na uwepo wake huyu ambaye amepewa majukumu ya kuwasimamia.
Carrick anatumia muda wake mwingi kuweza kufundisha illi aweze kufanikiwa kupata leseni A ya ukocha ya UEFA.

Carrick anamlisha anavyotaka, anampa uhuru anaojisikia na sasa Pogba anacheza soka la maisha yake akiwa na Manchester United.’





Share on Google Plus

About omary omary

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment