Kuelekea Liverpool vs Manchester United, haya ndio maneno ya Sadio Mane

1
Sadio Mane amesema ana furaha kubwa juu ya uamuzi wake wa kujiunga na Liverpool badala ya Manchester United, huku akikabiliwa na mchezo dhidi ya Mashetani Wekundu hao Jumatatu.
Meneja wa zamani wa United, Louis van Gaal alikaribia kumsajili Mane kutoka Southampton kwenda Old Trafford msimu uliopita.
Hata hivyo, badala yake Msenegal huyo aliamua kujiunga na Liverpool kuelekea msimu huu wa Premier League 2016-17 na kufanikiwa kufunga mabao matatu kwenye mechi sita mpaka sasa.
Huku Liverpool wakijiandaa kuwakaribisha United Anfield kesho, nyota huyo mwenye miaka 24 amefichua kwanini alikuwa sahihi kukataa ofa ya United.
“Kiukweli, kwa wakati ule kulikuwa na vilabu vingi vilivyokuwa vinanitaka lakini bado sikuwa nimefanya maamuzi,” Mane amesema na kuongeza. “Sikusema kwamba nilikuwa na fikra na klabu yoyote bali nilitaka kuendelea kucheza pale.
“Tetesi za kutakiwa na Liverpool zilinipa confidence kubwa uwanjani na kunifanya nizidi kujiamini, lakini nilijua hayo yote yametokea kwasababu ya uwajibikaji wangu na kwa hakika nilikuwa kwenye njia sahihi.
“Ronald Koeman hakuwa ba furaha kufuatia tetesi hizo kwasababu bado alikuwa akinihitaji, lakini halikuwa suala lilinipa mkanganyiko sana kwasababu kwangu ule haukuwa wakati wa kuondoka.
“Wakati nilipoongea naye nilimwambia, ‘Hakuna tatizo, nitaendelea kuwepo hapa’. Yalikuwa ni maamuzi yangu kubaki Southampton.
Nilikuwa na subira kwa kuwa baada ya mwaka mmoja nikiwa England nilifahamu ilikuwa vizuri zaidi kuelekeza nguvu zangu Southampton. Akilini mwangu, nilihisi ningebaki pale kipindi kirefu zaidi ili nifanye kitu kitakachothibitisha ubora wangu.
“Nilishawaishika kamba bado nilikuwa na muda wa kuthibitisha ubora wangu zaidi, kuimarika zaidi na kujifunza zaidi kabla ya kwenda kwenye klabu kubwa. Lakini nilijua fika muda gani hasa utakuwa sahihi kwangu.
“Mwaka uliofuata niliimarika zaidi na hiyo ni muhimu sana kwa kila mchezaji kwenda hatua kwa hatua.
“Wakati uliofika ndipo nilipoamua kwenda Liverpool na wakati wanaleta ofa yao sikuwa na muda wa kujiuliza mara mbili-mbili.”
Na hatimaye nimejiunga na Liverpool na nilikuwa na furaha kubwa, na mpaka sasa nina furaha pia ninaenda kucheza dhidi ya Manchester United.
Share on Google Plus

About omary omary

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment